ASSAs

JESHI LAZIDI KUWEKA JUHUDI KWENYE KOROSHO

1491
0
Share:

Jeshi la wananchi wa Tanzania limesema liko tayari kutumia meli yake yenye uwezo wa kubeba tani mia tano kusafirisha Korosho kwenda jijini Dar es Salaam baada ya maghala yaliyopo mkoani Mtwara kujaa.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo katika kikao chake na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mtwara.

Amesema katika ziara yake aliyoifanya kwenye maghala makuu ameshuhudia Korosho kujaa kwenye maghala hayo na kusema kuwa iwapo zitaendelea kukusanywa kwa wananchi jeshi litalazimika kutumia meli yake kupunguza sehemu ya Korosho ili ziweze kuifadhiwa jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo amesema upatikanaji wa maghala jijini Dar es Salaam, jeshi litalazimika kufanya mazungumzo na Wizara ya Kilimo ili kuona namna ya kuandaa maghala hayo kwa ajili ya kutunzia Korosho.

Akizungumza kuhusu ubanguaji wa Korosho, Jenerali Mabeyo amesema vikundi vya wabanguaji wadogo wa Korosho watatumika kubangua Korosho hizo na kikubwa kinachohitajika ni kuwaongezea nguvu kazi ya watu ili kazi hiyo iweze kufanyika haraka na kwa tija.

(Visited 169 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us