ASSAs

MBIVU NA MBICHI U 17 KUJULIKANA LEO

1425
0
Share:

Droo ya upangaji wa makundi ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 (AFCON) inatarajiwa kupangwa hii leo Jijini Dar es salaam.

Upangaji wa droo hiyo utafanyikia kuanzia saa 1:00 usiku katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, ukiratibiwa na Shirikisho la Soka barani Afrika CAF na Shirikisho la Soka Tanzania TFF ambao ndiyo wenyeji wa michuano hiyo.

Timu zilizofuzu kushiriki michuano hiyo ni pamoja na Mwenyeji, Tanzania, Angola, Cameroon, Guinea, Morocco, Nigeria, Senegal naUganda.

Fainali za michuano hiyo zinatarajia kufanyika kuanzia April 14 hadi 28, 2019 ambapo timu zitakazofuzu hatua ya nusu fainali, zitaliwakilisha bara la Afrika katika michuano ya Dunia ya vijana chini ya miaka 17 itakayofanyika mwakani nchini Peru.

(Visited 130 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us