ASSAs

‘MLIZALIWA WASHINDI’ DKT. MENGI

1738
0
Share:

Mlezi wa timu ya taifa ya soka ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi,  amewapongeza wachezaji hao kwa ubingwa wa COSAFA walioutwaa nchini Botswana.

Dkt. Mengi ametoa pongezi hizo leo Desemba 20, 2018 katika hafla ya chakula cha mchana alioyowaandalia vijana hao pamoja na viongozi wa TFF na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiongozwa na Waziri Harrison Mwakyembe.

Akiongea katika hafla hiyo Dkt. Mengi amesema, ”nyinyi mlizaliwa washindi na siku zote nalisema hilo, nawashukuru vijana wangu kwa kutekeleza ahadi ya kurudi na kombe hili kama mlezi wenu nimejisikia vizuri sana”, amesema.

Katika hafla ya chakula hicho cha mchana, nahodha wa Serengeti Boys, Michael Morris amemkabidhi mlezi wa timu hiyo Reginald Mengi zawadi maalum pamoja na mpira uliosainiwa na wachezaji wote.

Serengeti Boys ni timu pekee ya taifa ya Tanzania ambayo imekuwa na mwenendo mzuri katika michuano ya kimataifa ambapo mwaka huu wamefanikiwa kutwaa mataji mawili likiwemo lile la Afrika Mashariki na kati (CECAFA).

(Visited 233 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us