ASSAs

RC KAGERA ATUMA SALAMU KWA WAMACHINGA

915
0
Share:

Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti ametoa onyo kwa  wafanyabiashara wadogo ‘Machinga’ kuwa walinzi kwa kutoa taarifa ya wafanyabiashara ambao wameanza kupunguza bidhaa katika maduka yao kwa lengo la kupewa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo, huku ikisisitiza kuwa watakaobainika watachukuliwa hatua.

 Brigedia  Gaguti amezungumza  wakati akizindua rasmi zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo, lililofanyika katika manispaa ya Bukoba.

Gaguti amesema kuwa zipo taarifa kuwa baadhi ya wafanyabiashara wameanza kuhamisha bidhaa katika maduka yao, hivyo kuwataka wajasiriamali wadogo kuwa walinzi kwa kuwabaini na kutoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika ili hatua za haraka za kudhibiti udanganyifu huo ziweze kuchukuliwa.

Kwa upande wake meneja wa mamlaka ya mapato nchini (TRA) mkoa wa Kagera, Adam Ntoga, amesema kuwa utaratibu huo unawahusu wajasiriamali ambao hawajawahi kuingizwa katika mfumo wowote wa malipo ya kodi wa TRA, na ambao mzunguko wao wa mauzo ni chini ya shilingi milioni nne kwa mwaka, huku akielezea utaratibu utakaotumika kufanya malipo.

Mbali na Kagera, Uongozi wa Mchinga mkoani morogoro wamewataka wafanyabiashara wenzao kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu kwa kutumika na wafanyabiashara wakubwa kupata vitambulisho vya Rais kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria na kurudisha nyuma jitihada zake katika kuwajali wanyonge.

Mwenyekiti huyo, Faustine Frances amebainisha kuwepo kwa viashiria vya wafanyabiashara wakubwa kutaka kuingilia zoezi hilo kwa kupata vitambulisho hivyo kwa jia zisizo sahihi kwa lengo la kukwepa kodi jambo litakalopelekea serikali kukosa mapato.

(Visited 56 times, 1 visits today)
Share this post