ASSAs

RAMADHANI KABWILI ALAZWA

1691
0
Share:

Golikipa wa Yanga Ramadhani Kabwili, amelazwa katika hospitali ya Selian jijini Arusha akifanyiwa vipimo zaidi kufuatia maumivu ya nyonga aliyopata leo kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya  African Lyon iliyochezwa jijini Arusha

Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Samwel Lookmay, amesema Kabwili bado yupo hospitali madaktari wakiendelea kumfanyia uchunguzi ili kubaini ukubwa wa tatizo lake.

“Kabwili alipata matatizo kwenye nyonga na sasa hivi bado yupo chumba cha CT Scan akifanyiwa uchunguzi ili kugundua tatizo ni nini , lakini misuli ilibana na kupelekea kushindwa kabisa kuendelea na mchezo”, amesema Samwel Lookmay,

Aisha kaimu Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa kinachosubiriwa kwasasa ni taarifa kutoka kwa daktari ili kujua ni nini kitaendelea ama kama ataruhusiwa kutoka.

(Visited 177 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us