ASSAs

VYAMA PINZANI WAPINGA MAHAKAMANI

1515
0
Share:

Baada ya azimio la pamoja kwa viongozi wa vyama vya upinzani Zanzibar, wanatarajia kuhudhuria kesi inayowakabili Viongozi Wakuu na wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam inayotarajiwa kutajwa leo.

Kesi hiyo Na. 112/2018 inatarajiwa kuanza kusomwa asubuhi hii huku Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe pamoja na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wakitokea gereza la Segerea.

Viongozi ambao watahudhuria kesi hiyo ni, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-wazalendo, Zitto Kabwe na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif.

Viongozi Wakuu wa CHADEMA wanaokabiliwa na kesi hiyo ni pamoja na  M/kiti wa Chama Freeman Mbowe (Mb) KM Dkt Mashinji, NKMB Mnyika (Mb), NKMZ Salum Mwalim, Mkt wa BAWACHA Taifa Halima Mdee (Mb), John Heche (Mb), Ester Matiko (Mb) na Peter Msigwa (Mb).

Wanakabiliwa na kesi ya kula njama na kufanya mikusanyiko isiyokuwa ya halali iliyopelekea mwanafunzi wa chuo cha Usafirishaji NIT, Aqwiline Akwilini kupoteza maisha baada ya kupigwa risasi.

(Visited 181 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us