ASSAs

RATIBA YA LIGUU KUU SIMBA YABADILISHWA

1239
0
Share:

Bodi ya Ligi (TPLB) kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetangaza mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba vs Singida United kupigwa Disemba 29 badala ya 30.

Mabadiliko yamekuja kutokana na mmiliki wa Uwanja kusema utakuwa na matumizi ya kiserikali kwa siku za Disemba 30 na 31.

Mechi hiyo imerudishwa nyuma ambapo sasa itapigwa majira ya saa 1 kamili za usiku kwenye Uwanja ulele wa Taifa.

Wakati kabla ya mechi hiyo kupigwa, kikosi cha Simba kipo mawindoni kujiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa dhidi ya Nkana Red Devils kwenye Uwanja wa Taifa, Jumapili ya wiki hii.

Simba ianenda kucheza mchezo huo ikipaswa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 tu na isiruhusu nyavu zake kuguswa ili kufanikiwa kutinga hatua inayofuata.

(Visited 103 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us