ASSAs

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

1174
0
Share:
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kuwataarifu wasafirishaji na umma kwa ujumla kuwa Sheria ya Udhibiti wa Uzito wa Magari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Vehicle Load Control Act, 2016) na Kanuni zake za mwaka 2017 itaanza kutumika rasmi nchini Tanzania kuanzia tarehe 1 Januari, 2019. Tangazo la Sheria hii lilichapishwa kwenye Gazeti la Jumuiya ya Afrika Mashariki yaani “EAC Gazette – Legal Notes No. EAC/94/2016 tarehe 18 Novemba, 2016 na Kanuni zake kutungwa mwaka 2017. Wizara inatoa wito kwa wasafirishaji wote, watumiaji wa barabara na wadau wa Sekta ya Ujenzi na Usafirishaji kwa ujumla kuhakikisha kuwa wanaisoma na kuielewa vema Sheria ya Udhibiti wa Uzito wa Magari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kanuni zake inayopatikana katika tovuti ya Wizara (www.mwtc.go.tz), ili kuepuka adhabu zinazoweza kutolewa kwa kukiuka Sheria hiyo. Aidha, wasafarishaji wote nchini wanatakiwa kutii na kuzingatia kikamilifu matakwa ya Sheria hiyo kwa kutozidisha uzito wa magari ili kuzifanya barabara zetu zidumu kwa muda mrefu. Kufuatia kuanza utekelezaji wa Sheria hiyo, ukomo wa uzito wa mtaimbo (Axle) wenye matairi mapana (Super Single Tyres) utakuwa tani 8.5 badala ya tani 10 za sasa; tani 16 badala ya tani 18 kwa mitaimbo miwili (Tandem Axles); na tani 22.5 badala ya tani 24 kwa mitaimbo mitatu (Trindem Axles). Hata hivyo, ukomo wa uzito wa jumla wa magari (Gross Vehicle Mass – GVM) utabakia kuwa tani 56, hivyo wasafirishaji
 
wanashauriwa kupanga vizuri mizigo kwenye magari ili kuepuka adhabu ya uzidishaji uzito kwenye mitaimbo (axles). Wasafirishaji watakaohitaji kusafirisha mizigo isiyokuwa ya kawaida watatakiwa kuomba vibali vya kusafirisha mizigo hiyo Wizarani kupitia mtandao wa e-permits kama ilivyo sasa ambao unafanya kazi 24/7.
 
Vibali vya kusafirisha mizigo isiyokuwa ya kawaida vitakuwa katika makundi matano (5) kama ifuatavyo:
 
(i) Abnormal Load (mzigo uliozidi vipimo kwa mujibu wa
 
Sheria).
 
(ii) Awkward Load (mzigo ambao unaweza kugawanyika lakini
 
unahitaji umakini zaidi na vifaa maalum katika ushushaji wake).
 
(iii) Hazardous Load (mizigo hatarishi kwa afya na usalama
 
katika usafirishaji wake kwa njia ya barabara).
 
(iv) Super Load (mzigo ambao haugawanyiki na umezidi kiwango
 
cha uzito unaoruhusiwa kisheria).
 
(v) Unstable Load (mzigo ambao unaweza kuhama kutoka
 
sehemu moja ya gari hadi sehemu nyingine wakati gari likiwa kwenye mwendo au limesimama).
 
Vibali vya kusafirisha mizigo isiyokuwa ya kawaida vitalipiwa Dola za Kimarekani 10 (USD 10) badala ya Dola za Kimarekani 20 (USD 20) kwenye Sheria inayotumika sasa.
(Visited 113 times, 1 visits today)
Share this post