ASSAs

BASHE : TUMEFANIKIWA KUANZA UJENZI WA ZAHANATI

477
0
Share:

Nzega mjini

Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Hussein Bashe amesema katika muda wa miaka mitatu wamefanikiwa kuanza ujenzi wa Zahanati na vituo vya Afya kwa kata zote zilizo mbali na mji, jambo hili limeenda sanjari na ujenzi wa nyumba za watumishi wa Afya katika maeneo mengi.

Amesema kuwa, ujenzi wa kituo cha afya cha kisasa cha Zogolo kinaacha alama kama moja ya mafanikio makubwa katika sekta hii ndani ya jimbo hilo, lengo likiwa ni kupunguza adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kufata huduma za Afya.

Aidha amesema wamefanikiwa kuihamisha hospital ya Wilaya ya Nzega kutoka Halmashauri ya Wilaya na kuja Halmashauri ya Mji ambapo kwa kushirikiana na Serekali ambapo wameweza kuongeza wodi za wagonjwa pamoja na vifaa tiba.

(Visited 27 times, 1 visits today)
Share this post