ASSAs

MAULID KITENGE AMSHUSHIA USHAURI DIAMOND, JIPANGE!!

1920
0
Share:

Mtangazaji maarufu wa habari za michezo hapa Tanzania, Maulid Kitenge ametoa ushauri wake kwa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kufuatia show yake aliyoifanya kwenye tamasha la Wasafi Festival nchini Kenya.

 Mtangazaji Maulid Kitenge.

Kitenge ametoa maoni hayo kwenye ukurasa wake wa Twitter, ambapo amemtaka Diamond awamu ya pili akienda Kenya atumie muda mwingi kuimba kuliko kuwaimbisha mashabiki wake au kutumia playback.

 

Siku ya jana Jumatatu nchini Kenya kuliibuka mijadala mizito kwenye mitandao ya kijamii ikizungumzia kuhusu show ya Wasafi Festival iliyofanyika Kenya Jumatatu ya Desemba 31, 2018, wengi wakisema kuwa Diamond aliboa jukwaani.

Wadau wengi wamesema kuwa Diamond na baadhi ya wasanii waliboa jukwaani, kwani walitarajia kuona vitu vikubwa kutoka kwao lakini jukwaani hawajaonesha kiwango stahili.

(Visited 289 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us