ASSAs

“MIMI NA AUNTY NI WANANDOA BADO SHEREHE TU”- IYOBO

1535
0
Share:

Mpenzi wa Msanii wa filamu za Bongo movie Aunty Ezekiel, Mose Iyobo ameibuka na kuweka wazi kuwa yeye na mama Watoto Wake Aunty Ezekiel ni Kama wanandoa bado kufanya sherehe tu.

Mose Iyobo ambaye ni mcheza shoo wa Diamond Platnumz amesema kuwa watu wamekuwa wakimuuliza sana lina atafunga ndoa na Aunty Ezekiel Lakini yeye anaona wao wawili ni kama wanandoa tayari kilichobaki ni kufanya harusi tu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers Mose Iyobo aliulizwa ni lini atafunga ndoa na Aunty ambaye tayari Ameshazaa naye Mtoto mmoja ambaye anaitwa Cookie:

Kwa jinsi tunavyoishi ni ndoa tayari kwa sababu tunakaa pamoja, Mungu ametujalia mtoto mzuri (Cookie), yaani sisi ni kama wanandoa bado sherehe tu ambayo muda wowote tutafanya wala haina haraka“.

Lakini pia Iyobo amekataa kabisa tetesi zilizosambaa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa yeye na Aunty wameachana:

Mimi na Mama Cookie hatujawahi kuachana ila tumeshawahi kupishana kauli zaidi ya mara mbili na huwa tunamaliza tofauti zetu wenyewe na maisha yanaendelea“.

(Visited 152 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us