ASSAs

UMMY MWALIMU AKABIDHI BATI 100 TANGA

1026
0
Share:

Tanga

Mbunge wa wilaya ya Tanga (CCM Viti maalumu) ambae pia ni Diwani wa kuapishwa (kura) Jiji la Tanga, Ummy Mwalimu ametoa mabati 50 ya kuezekea Boma la Zahanati ya Mapojoni lililojengwa kwa Nguvu za wananchi.

Aidha Mbunge huyu wa wa CCM – Tanga, aliwasili katika ujenzi wa Bweni la Wasichana lililojengwa kwa nguvu ya wananchi wa kale pia amekabidhi mabati 50 ya kuezekea jengo hilo , Mara tu baada ya kushiriki ujenzi huo.

Katika hatua nyengine Ummy Mwalimu alizungumza na wananchi wa Mapojoni na Kirare, hali ilioyowavutia wananchi na kiongozi wa (CDM) Katibu mwenezi kata kirare) alitelemsha bendera za chama chake kutokana na imani ya uchapaji kazi wa Ummy.

(Visited 66 times, 1 visits today)
Share this post