ASSAs

LIVERPOOL YATOLEWA MICHUANO YA FA

827
0
Share:

Klabu ya Liverpool kutoka nchini Uingereza imeanza kutetereka baada ya kufungwa na klabu ya Wolverhampton Wanderers katika michuano ya FA ambayo ni michuano ya pili kwa ukubwa hapo nchini kwao.

Kufungwa huko kwa Liverpool kumeifanya kutolewa katika michuano hiyo kwa kipigo cha jumla ya goli 2-1 licha ya kuwa ugenini.

Ikumbukwe kwamba Liverpool sasa hivi inashiriki katika michuano miwili tu ikiwa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya UEFA na Ligi kuu nchini kwa PL baada ya kutolewa kwenye michuano mingine inayofanyika hapo inayojulikana kama Carabao cup.

Liverpool ilifanikiwa kucheza michezo zaidi ya 19 ya ligi kuu nchini humo bila kupoteza hata mchezo lakini mchezo wake dhidi ya Manchester City ndio ukawa mchezo wake wa kupoteza wa kwanza kwenye ligi ambao ulikuwa mchezo wa 21.

Usiku wa kuamkia jana Majogoo Liverpool wakapoteza mchezo mwingine baada ya kufungwa na klabu ya Wolverhampton Wanderers, ingawa ilikuwa ni kwenye michuano mingine sio ligi yaani michuano ya FA na Liverpool kupoteza huko kumepelekea kutolewa katika mashindano hayo.

(Visited 51 times, 1 visits today)
Share this post