ASSAs

MAWIMBI YA RADIO ANGA ZA JUU YAGUNDULIWA NA WATALAAMU

747
0
Share:

Wataalamu wa anga za juu wamefichua kwamba walinasa mawimbi ya redio ya ajabu ambayo yalikuwa yanatoka mbali sana katika anga za juu.

Mawimbi hayo yalinaswa na darubini ya kufuatilia mawimbi ya redio ambayo ipo Canada na yanaaminika kutoka kwenye mfumo wa nyota na sayari ulio mbali sana.

Chanzo halisi cha mawimbi hayo ya redio bado hakijabainika na wala wataalamu hao hawajafahamu sifa kamili za mawimbi hayo.

Miongoni mwa mawimbi hayo ya redio ya kasi sana (yanayofahamika pia kama FRBs kwa maana ya Fast Radio Bursts), ambayo yalinaswa mara 13, kulikuwa na mawimbi yasiyo ya kawaida yaliyokuwa yakijirudia tena na tena. Yanaaminika kutoka kwenye chanzo kimoja umbali wa takriban miaka 1.5 bilioni kwa miaka ya kasi ya mwanga.

Tukio kama hilo limewahi tu kuripotiwa mara moja tu awali, na darubini tofauti.

“Kufahamu kwamba kuna nyingine imepatikana ni jambo linalodokeza kwamba kunaweza kuwa hata na zaidi,” amesema Ingrid Stairs, ambaye ni mtaalamu wa fizikia ya anga za juu katika Chuo Kikuu cha British Columbia (UBC).

“Na tukiwa na mitambo zaidi ya kuimarisha nguvu za mawimbi hayo na pia vyanzo vingi, basi tunaweza tukafahamu na kutanzua kitendawili hiki cha anga za juu – tujue mawimbi haya yanatokea wapi na nini chanzo chake.”

Kituo cha kutafiti anga za juu cha CHIME, kinachopatikana katika Bonde la Okanagan katika eneo la British Columbia, kina antena nne (waya maalum za kupokelea mawimbi ya sauti) za urefu wa mita 100 ambazo hufuatilia anga ya kaskazini kila siku.

Darubini iliyotumiwa ilianza tu kufanya kazi mwaka jana, na iliyanasa mawimbi hayo 13 ya redio karibu mara moja, pamoja na mawimbi hay ya kujirudia.

(Visited 47 times, 1 visits today)
Share this post