ASSAsSamaki Samaki

HII NDIO HOTELI YA KIFAHARI NCHINI ETHIOPIA NA YA KWANZA YENYE MGAHAWA WA KICHINA

316
0
Share:

bonizacharia.bz@gmail.com

Addis Ababa. Taarifa kutoka tovuti ya Aeronautical inaeeleza kuwa Hotel ya Skylight yenye hadhi ya nyota tano inayotarajiwa kufunguliwa mnano Januari 28, 2019 imejengwa kwa gharama kutoka kwa mashirika ya ndege ya nchini humo na benki ya Exim ya kichina.

Hoteli hiyo iliyo umbali wa dakika tano kutoka uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Addis Ababa yenye upana wa meta 42,000 na vyumba 373 inakadiriwa kugharimu kiasi cha dola 65,000,000 na hivi karibuni baada ya uzinduzi itazalisha ajira zaidi ya 400.

Kiasi hicho cha pesa, mtandao huo umeripoti kuwa mashirika ya Ndege ya Ethiopia yamechangia asilimia 35% ya kicha hicho cha pesa, huku asilimia 65% zilizobakia zimechangiwa na Benki ya China ya Exim.

Ukiachilia mbali faida ya Hoteli hiyo kukuza Utalii, pia itasaida kukaribisha abiria wakati wa kusafiri na kuwarahisishia huduma ya malazi ili kuepusha ucheleweshaji wa kiufundi, hii kwa mujibu wa shirika hilo la ndege la Ethiopia.

Skylight Hotel Ethiopia itakuwa ni miongoni mwa Hotel kubwa zinazomilikiwa na Kampuni ya Grand Skylight Hotel Management Co. Ltd inayosimamia Hotel zenye jina hilo katika miji mbalimbali mikubwa Nchini china kama, Grand Skylight CATIC Hotel mjini Beijing, Grand Skylight Hotel Yuayeng , Wanyue Grand Skylight Hotel Shenzhen, Grand Skylight Hotel Kaimei, Grand Skylight Hotel Yangzhou na nyingine nyingi na Sasa Grand Skylight Hotel in Addis Ababa Eithiopia.

Sehemu ndogo ya taarifa iliyoandikwa na mwandishi Chen Jingchun ya mnamo Juni 6, 2017 ilieleza kuwa Timu kutoka Usimamizi wa Grand Skylight Hotel ilitembelea Ethiopia na kufabya utafiti wa siku 6 wa eneo la kuanzisha mradi huo wa Grand Skylight Hotel wa Ethiopia Airlines.

Na baadae taarifa kutoka mtandao wa kampuni hiyo Grand Skylight Hotel Management Co. Ltd ulieleza kuwa,
“Tumeunda uzoefu ambao hutoa thamani kwa mgeni, kwa wafanyakazi, na kwa biashara, hadi kwa undani zaidi, utaalamu wetu unafikia kila eneo, mazingira ya biashara na kubuni kwa ufanisi wa usimamizi na muundo”,

“Huduma za wageni ambazo zinagusa moyo, huduma ya waajiri, mafunzo na motisha pamoja na dhana za biashara, na burudani na wamekutana ili kuunda eneo la kweli la kihistoria kwa msafiri wa biashara”.

Pia sehemu ya taarifa hiyo ilisema, “maelezo yote ya uendeshaji wa kila hoteli kwa uzuri, ni pale thamani ya kweli ya mali ya Grand Skylight inaangaza. Utunzaji mzuri na ushirikiano wa neema ni ufunguo wa mafanikio na inatuwezesha kutoa uzoefu wa kukubalika na kukubalika zaidi kwa wageni.

Hali kadhalika August 18, 2018 Kuputia ukurasa wa One Ethiopia kwenye mtandao wa Youtube kilipakiwa kipande kidogo kikionesha hatua za mwisho kahisa za ukamilifu wa Hoteli hiyo inayotarajiwa kufunguliwa Januari 28, 2019 kama ilivyoelezwa hapo mwanzo
Source: Grand Skylight Hotel, One Ethiopia.

(Visited 43 times, 1 visits today)
Share this post