MAHAKAMA YAWAFUTIA KESI KITILLYA NA WENZAKE

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia mashtaka aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Harry Kitillya, maofisa wawili wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kueleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri lao.
Kabla ya kukamatwa tena, Wakili Mkuu wa Serikali, Hashimu Ngole akisaidiana na wenzake Pendo Mangole na Patrick Mwida, amedai kuwa DPP hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa.
“Taarifa hii ya kutokuendelea na shauri hili mbele ya mahakama yako, imeletwa chini kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002,” amesema Ngole. Baada ya maelezo hayo,
Hakimu Ally alisema kutokana na maombi hayo, mahakama hiyo imeifuta kesi hiyo, hata hivyo walikamatwa mara tu baada ya kuachiwa, na pelekwa tena mahabusu.