ASSAsSamaki Samaki

‘MHE. RAIS MAGUFULI UMENIKOSHA’ ASKOFU KAKOBE

229
0
Share:
Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Askofu Zakaria Kakobe amemueleza Rais Magufuli kuwa amemkosha kutokana na hatua ya serikali kununua ndege mpya.

Akofu Kokobe amesema hayo wakati wa mapokezi ya ndege mpya aina ya Airbus 220-300 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julias Nyerere, Dar es Salaam.

“Mimi huwa ni mbishi kidogo na ukiniona nimekanyaga mahali kama hapa ujue Mh Rais Magufuli umenikosha,” amesema Askofu Kakobe.

Utakumbuka serikali katika jitihada za kufufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) hadi sasa serikali imenunua ndege aina ya Bombardier Q400 tatu, pamoja na Boeing 787-8 Dreamliner na Airbus 220-300, na leo imewasili nyingine aina ya Airbus 220-300.

(Visited 19 times, 1 visits today)
Share this post