ASSAsSamaki Samaki

MOURINHO MBIONI KURUDI MADRID

175
0
Share:

Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania wapo katika mikakati ya kumrudisha meneja wao wa zamani, Jose Mourinho katika anga ya Bernabeu, hata hivyo watalazimika kuilipa Manchester United Euro milioni 10m ikiwa watamuajiri.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni wiki chache tangu Jose mourinho kutumuliwa na Klabu ya Manchester United nchini Uingereza kutokana na mfululizo wa matokeo mabovu Uwanjani.

Utakumbuka Kocha huyo mbwatukaji alikinoa kikosi cha Real Madrid kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2010 hadi 2013 ambapo aliwezesha timu hiyo kutwaa mataji mbalimbali likiwemo la Ligi kuu nchini Hispania.

(Visited 9 times, 1 visits today)
Share this post