ASSAsSamaki Samaki

WAZAZI KUTOSHIRIKI VIKAO VYA MAENDELEO YA WANAFUNZI YAKWAMISHA KUPATA MATOKEO CHANYA

265
0
Share:

Dar es Salaam

Licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika shule ya Sekondari Vingunguti, wazazi kutoshiriki katika vikao vya maendeleo ya wanafunzi imetajwa ni sababu ya wanafunzi hao kufanya vibaya katika mitihani yao licha ya juhudi mbalimbali zinazofanywa shuleni hapo.

Hayo yameelezwa mapema leo na Mwalimu wa sekondari Vingunguti wa Shule hiyo Shija Fumbuka wakati alipotembelewa na Afisa Utumishi Mkuu wa Benadetha Mwaikambo pamoja na Diwani wa kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto lengo ikiwa ni kusikiliza kero za walimu waliopo shuleni hapo, ambapo shule hiyo ina wanafunzi wengi ikilinganishwa na vyumba vya madarasa vilivyopo.

Aidha amesema, chumba kimoja wanakaa wanafuzi 954, hivyo walimu wa shule hiyo hulazimika kuandaa mikutano lengo ni kuangalia changamoto gani zinapelekea wanafunzi hao kufanya vibaya katika mitihani lakini wazazi wanakua hawaitikii wito na badala yake hali hiyo kujirudia.

Jengo la shule ya Sekondari Vingunguti

“Ni kweli shule yetu inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa madawati, maabara, vyumba vya madarasa, geti, uzio pamoja na uchavu wa miundombinu lakini na wazazi kutoshiriki katika vikao vya maendeleo ya wanafunzi inachangia watoto wetu kufanya vibaya ” amesema Fumbuka

Kwa upande wake Afisa Utumishi Mkuu Benadetha Mwaikamba amesema kuwa, changamoto zote zilizowasilishwa na walimu hao atazichukua na kuzifanyia kazi na ambayo yapo nje ya uwezo wake atayapeleka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne kiangio saidi

“Leo nimekuja katika shule hii ya Sekondari Vingunguti lengo kuskiliza kero za walimu, nashukuru wamekua wa wazi wameelezea dhamira yao lakini kuna maboresho mbaya yanhitajika ili kuweza kuwapa motisha ya kutoa elimu yenye ubora zaidi ” amesema Mwaikamba

Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto amesema, kata hiyo imekua na changamoto nyingi, hivyo anawaomba wadau mbalimbali wa maendeleo kuona ni namna gani wanaweza wakatoa msaada wao wa hali na mali ili kuhakikisha wananchi wa kata hiyo wanaishi katika mazingira rafiki.

“Changamoto ni nyingi zilizopo shuleni hapa nimezibeba ambazo zipo ndani ya uwezo wangu nitaenda kuzifanyia kazi, hizi nyengine lazima tushirikiane na wazazi pamoja na wadau ili kuzitatua ” amesema Kumbilamoto

(Visited 46 times, 1 visits today)
Share this post