ASSAsSamaki Samaki

AHUKUMIWA MIAKA 7 JELA KWA KENDESHA BIASHARA YA UPATU

248
0
Share:

​Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu Jones Moshi(42) na James Gatuni(35) Mkenya, kulipa faini ya Sh. milioni 204 au kwenda jela miaka 7 kwa kosa la kuendesha biashara ya upatu na utakatishaji fedha

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, alisema katika kosa la kwanza la utakatishaji fedha kila mmoja anatakiwa kulipa faini ya Sh. milioni 2 na endapo watashindwa kufanya hivyo watatakiwa kutumikia kifungo cha miaka 2 gerezani

Mashauri alisema katika shtaka la pili linalohusu utakatishaji fedha haramu kila mshtakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh. milioni 100 na endapo atashindwa kufanya hivyo atalazimika kutumikia kifungo cha miaka 5 jela

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Shadrack Kimaro akisaidiana na Wakili Esther Martine na Neema Mbwana walidai Mahakamani hapo kuwa wawili hao walitenda kosa hilo kati ya Julai 14 mwaka 2014 na March 31 mwaka 2016, jijini Dar es Salaam na maeneo mbalimbali Tanzania.

(Visited 30 times, 1 visits today)
Share this post