ASSAs

BINGO KARATA YA KWANZA YA SIMBA , YA MABINGWA BARANI AFRIKA.

1356
0
Share:

Mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Mabingwa barani Afrika leo tarehe Januari 12, 2018 umechezwa katika uwanja wa Taifa Jijin Dar es salam kati ya Simba Sc ya Tanzania dhidi ya Js Saoura ya Algeria na kumalizika kwa Simba Sc kuibuka na ushindi wa magoli 3:0 dhidi ya wageni wao, Goli moja likifungwa katika kipindi cha kwanza na mawili kipindi cha pili.

Katika mchezo huo ulioanza majira ya saa 10 alasiri, Simba walianza kipindi cha kwanza kwa mashambulizi yalioonekana kuwachanganya wageni licha kuwa mashambulizi hayo hayakuwapatia Simba bao lolote kwa dakika 45 za mwanzo kabla ya kuongezwa dakika 3 zilizompa nafasi Emmanuel Anord Okwi kuipatia Simba goli la kwanza na kwenda mapumzikoni wakitamba.

Mashambulzi kadhaa kipindi cha kwanza yalionekana kuwapa wakati mgumu Js Saoura kwani hayakuwapa nafasi ya kupumua hata Takwimu zilidhibitisha hilo na kuwafanya Simba wautawale mchezo, Shambulizi la dakika ya 19 Emmanuel Okwi aliachia shuti kali lililogonga mwamba moja kwa moja na kurudi uwanjani baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Pascal Wawa.

Shambulizi lingine Dakika ya 34 Pia halikuleta matokeo, lakini Simba wameendelea kuonyesha nia ya kutaka matojeo mazuri na hatimae dakika ya 45+3 kupitia kwa mshambuliaji Okwi Ubao umebadilika kuwa 1:0 na kwenda mapumzikoni wakiwa wanatamba.

Kipindi cha pili kilianza kama kilivyoanza kipindi cha kwanza kwa Simba kushambulia kwa kasi na hali hiyo kusaidia kujipatia goli la pili dakika 51 kupitia kwa Meddie Kagere (Mk 14) kwa kumalizia pasi safi kutoka kwa Emmanuel Okwi na dakika 16 baadae Mk 14 kwa mara nyingine tena anakamilisha kalamu ya magoli matatu yalidumu mpaka dakika za mwisho mwamuzi alipopuliza kipenga kuashiria kumalizika kwa dakika 90+3 za mchezo huo.

Kwa matokeo hayo Simba inakuwa timu kiongozi ikiwa na pointi 3 na magoli 3 katika Group D lenye timu ambazo ni Simba Sc, Al Ahly, Vita Club na Js Saoura.

 

(Visited 114 times, 1 visits today)
Share this post