ASSAsSamaki Samaki

MWENYEKITI WA CCM WA IRINGA AFANYA ZIARA KATIKA CHUO CHA VIJANA IHEMI

255
0
Share:

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Dkt.Abel Nyamahanga Afanya ziara na kukagua Chuo cha Vijana wa CCM Ihemi.

katika ziara hiyo ameongozana na baadhi ya Viongozi wa Secretariati ya CCM Mkoa, alifika Chuoni hapo na kusaini Vitabu kisha kukagua maeneo yote ya Chuo ikiwa ni pamoja na Maeneo yote yatakayowekwa Miradi mikubwa ya Kilimo na Ufugaji,
Amekagua Majengo yote, na kuzungumza na watumishi waliopo Chuoni hapo.

Pia aliweza kukagua shughuli ya Uchimbaji wa Msingi na uwekaji wa bomba za maji kwenye eneo hilo zoezi linalosimamiwa na Wizara husika.

Aidha amewapongeza watumishi walipo Chuoni hapo,hasa katika juhudi zinazofanywa na Umoja wa Vijana,
pia amesema Jitihada kubwa zinazofanywa na Viongozi wa Chama hicho  chini ya usimamizi wa Dkt.Bashiru Ally katika kuhakikisha Chuo cha Ihemi kinarudi katika misingi iliyotarajiwa.

(Visited 23 times, 1 visits today)
Share this post