ASSAs

TAARIFA YA KUUNGUA KWA BWENI LA SHULE YA SEKONDARI MLANGARINI LEO ASUBUHI

854
0
Share:

Leo tarehe 12/01/2019 Majira ya Saa 07:02 asubuhi mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro amethibitisha kupokea taarifa za tukio la kuungua Kwa Bweni la wavulana la shule ya Sekondari Mlangarini Ambayo ni shule ya Serikali iliyo katika kata Mlangarini Halmashauri ya Arusha Wilaya ya Arumeru .

Taarifa za Awali zinaeleza Moto huo ulianza majira ya Alfajiri na kuteketeza chumba Kimoja kati ya vyumba kumi na nne vya bweni hilo lililokuwa na wanafunzi 84 Hakuna majeruhi wala vifo , japo Kuna uharibifu wa Mali ikiwemo Kuungua kwa vitanda (double) vitatu (3),magodoro (6),Masanduku ya Kuhifadhia Nguo na Madaftari

DC Muro amesema Kutokana na changamoto hiyo alilazimika kufika kwenye Eneo la tukio mapema na kuungana na wanafunzi pamoja na wananchi waliojitokeza katika hatua za awali ambapo pia kikosi cha Zimamoto kiliwahi kufika kwenye eneo la tukio na kukuta moto umezimwa kwa ( fire extinguisher 11).

(Visited 71 times, 1 visits today)
Share this post