ASSAs

WATUMISHI WA MUNGU WAMPONGEZA MABULA KUWA KIONGOZI ANAYEISHI AHADI

862
0
Share:

Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ametajwa kuwa ni miongoni mwa wakilishi wananchi wachache nchini wanyenyekevu wenye chapa halisi ya utumishi unaoishi ahadi kwa kuzitekeleza kwa vitendo.

Haya yamebainishwa na ujumbe wa mtumishi wa Mungu wa kimataifa Mchungaji Nathan Thuber kutoka huduma ya Toronto International Celebration nchini Canada aliyemtembelea Mhe. Mabula ofisini kwake Nyamagana akiwa na ujumbe wa kutoka Umoja wa makanisa ya Kikristo kutoka Kamati ya Amani ya mkoa wa Mwanza Askofu Sekerwa pamoja na Askofu Isaya.

Mchungaji Thumber ambaye yupo mkoani Mwanza kwaajili ya maandalizi ya mkutano mkubwa wa Injili hapo Juni 2019, amepata fursa ya kuliombea taifa la Tanzania na uongozi wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe pamoja na mbunge Jimbo la Nyamagana.

(Visited 71 times, 1 visits today)
Share this post