ASSAsSamaki Samaki

WAZIRI UMMY ATOA VIFAA VYA UJENZI WA MADARASA YA SHULE YA SEKONDARI TANGA

240
0
Share:

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga, Ummy Mwalimu amechangia Tofali 3,500, Saruji Mifuko 250 lengo ni kusaidia ujenzi wa madarasa katika Shule za Sekondari 5 za Jiji la Tanga.

“Kazi ya kuijenga Tanga nimechangia Tofali 3,500, Saruji Mifuko 250 kusaidia ujenzi wa Madarasa katika Shule za Sekondari 5 za Jiji la Tanga ambazo ni Pongwe, Maweni, Mikanjuni, Horten na Kiomoni ambapo kila shule nimeipatia Matofali 700 na saruji mifuko 50″Waziri Ummy

Amesema kuwa, jitihada za Mhe Rais Dr. John Pombe Magufuli za kuboresha Elimu nchini, zimewezesha ongezeko la ufaulu wa wanafunzi walio na sifa ya kujiunga na Kidato cha Kwanza. Jiji la Tanga wanafunzi wameongezeka kutoka 5,332 mwaka 2018 hadi wanafunzi 6,024 mwaka huu 2019.

“Hali hii imesababisha mahitaji ya ziada ya Vyumba vya madarasa 71 ili kumudu kuchukua ongezeko la wanafunzi 1,324 waliofaulu kwenda Sekondari katika Jiji la Tanga”amesema Waziri Ummy

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji ameahidi kuwa Halmashauri itatoa pesa ya ufundi shilingi milioni 5 kwa shule zote 5 nilizozipatia vifaa vya ujenzi ili ujenzi wa madarasa hayo ukamilike haraka.

(Visited 23 times, 1 visits today)
Share this post