ASSAs

KATIBU WA CHADEMA WILAYA YA MBEYA MJINI AJIVUA UWANACHAMA

950
0
Share:

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Mbeya Mjini, kimepata pigo baada ya Katibu wake, Raphael Mwaitege, kutangaza kujivua nyadhifa zake zote ndani ya chama hicho pamoja na uwanachama akidai kuwa anataka kupumzika siasa.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini humo, Mwaitege amesema kuwa amefikia uamuzi huo ili kuokoa maisha yake kutokana na vitisho alivyokuwa anavipata kutoka kwa wanachama wenzake wa chama hicho ambao walikuwa wanamtishia maisha.

Naye Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mbeya Mjini, Agustino Mwadalu amesema chama hicho kiko tayari kumpokea mwanachama yeyote wa upinzani ambaye ni msafi na anataka kuhamia katika chama hicho kwa ajili ya maendeleo.

Ninamkaribisha ndugu yangu Katibu wa Chama wa CHADEMA, awe huru, aje kwenye chama ambacho kina sera, chama ambacho kina upendo na kwenye chama ambacho kimechukua dhamana ya kuwaongoza Watanzania, chama kinachoishi na Watanzania na kinachoongoza kwa m,ujibu wa sheria“, amesema Katibu huyo wa CCM.

Kabla ya Mwaitege kutangaza uamuzi huo, Mwezi Julai mwaka jana Chadema kilipoteza madiwani wanne ambao walihamia CCM akiwemo aliyewahi kuwa Naibu Meya wa kwanza kupitia chama hicho, David Ngogo.

(Visited 51 times, 1 visits today)
Share this post