ASSAs

DSTV WAKISHIRIKIANA NA SPORT PESA WAZINDUA MSIMU WA TATU WA MASHINDANO YA SPORT PESA

1062
0
Share:

Kampuni ya Malti Choice wakishirikiana na Sport Pesa Januari 15, wamezindua msimu wa tatu wa mashindano ya sport pesa ambapo mashindano hayo yatashirikisha timu kutoka Kenya na Tanzania na yanatarajia kuanza tarehe 22 januari hadi tarehe 27 mwezi huu katika uwanja wa Taifa.

Ushirikiano huo umekuja baada ya makubaliano yaliyofanywa na kampuni zote mbili kuwa mashindano hayo yaonyeshwe kupitia chaneli ya super sport namba 9.

Akizungumza nawaandishi wa habari januari, 16,2019 jijini Dar es Salaam Salum meneja Masoko wa Malti Choice Ronald Baraka Shelukindo  amesema Kuelekea msimu wa tatu wa Sport pesa kampuni ya maltchoice Tanzania imewaondoa wasiwasi wadau na wapenzi wa mpira wa miguu juu ya ubora wa picha na urushwaji wa matangazo kupitia visumbusi vya Dstv kuwa utakua ni wakimataifa hivyo wajipange kuburudika na msimu wa tatu wa sportpesa kupitia chaneli namba 9 inayopatikana kwenye vifurushi vyote vya Dstv.

“Tunaujali ushirikiano wenu waandishi na pili sina shaka na nguvu iliyowekwa na SportPesa na natumaini timu zetu kubwa hapa Tanzania hazitakuja zikiwa na Mapungufu, na nawahakikishia hakutakuwa na shaka ya quality Transmission, na naomba waandishi mlifikishe kwa wananchi kama lilivyo na kusisitiza kuwa wakati huu utakuwa mzuri sana… Tarimba ananikumbusha kuwa mshindi atacheza na Everton tena kwa nchi ambayo anatokea” amesema Shelukindo.

Aidha kampuni ya sports pesa kupitia mashindano ya sport pesa msimu wa tatu wametoa idadi ya timu zitakazo shiriki mashindano hayo ambazo ni Bandari fc,Fc Leopard na Gor mahia Cariobangi sharks kutoka Kenya na Mbao fc Simba fc Singida United na Young Afrika kutoka Tanzania watakacheza mechi tatunkwa kila timu kufikia fainali ambapo mshindi atacheza na Everton kutoka uingereza.

“Tulikua na mazungumzo mazito na vilabu vyetu vya hapa Tanzania, safari hii hatuhitaji mchezo mchezo, tunahitaji wawe serious ili kupata fursa ya kucheza na moja ya vilabu vikubwa barani Ulaya”.amesema  Tarimba

 

(Visited 92 times, 1 visits today)
Share this post