ASSAs

SPIKA WA BUNGE LA KENYA ASEMA HAKUNA NCHI INAYOWEZA KUJISIFU KWA DEMOKRASIA

1731
0
Share:

Spika wa Bunge la Kenya Mhe. Justin Muturi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge nchi Wanachama wajumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA AFRICA REGION) (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo. Kulia ni Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai.

MWENYEKITI wa Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wabunge Wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA Afrika Region) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Kenya Justin Mutiri amesema hakuna nchi yoyote duniani ambayo inaweza kusimama na kujisifu kuwa demokrasia yao ndio nzuri zaidi ya nchi nyingine.Ametoa kauli hiyo leo Januari 17, 2019 jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa habari kuhusu kikao cha Kamati hiyo ambapo pamoja na mambo mengine watajadili bajeti ya Bunge hilo pamoja na kuangalia hali ya demokrasia na haki za binadamu.Tumekutana jijini Dar es Salaam na tangu juzi tumekuwa na vikao kujadili masuala mbalimbali pia tutaangalia bajeti na maeneo gani ya kupewa kipaumbele.Pia tunaangalia demokrasia na haki za binadamu kwani nayo ni miongoni mwa mambo ambayo tunayapa kipaumbele katika nchi za Afrika,”amesema Mutiri.

Alipoulizwa kuhusua hali ya demokrasia kwa nchi ya Afrika ikoje? Spika huyo wa Bunge la Kenya amejibu kuwa kila nchi ina namna ya kufanya demokrasia ya yake, hivyo huwezi kuzungumzia moja kwa moja kuhusu demokrasia.Huwezi kukaa na kusema demokrasia yangu ndio nzuri zaidi kuliko sehemu nyingine.Hivyo hakuna nchi yoyote duniani ambayo inaweza kujisifu kuwa inaongoza katika masuala ya demokrasia.Ameongeza kuwa hivyo wanapozungumzia suala la demokrasia kwa Afrika wanaizungumza kwa upana wake na kubwa zaidi demokrasia ambayo ni nzuri ni ile ambayo inaleta ustawi wa maendeleo kwa wananchi wote.

Kuhusu Kamati yao kukutana jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, Mwenyekiti huyo amefafanua wanayofuraha kuwa nchini kwani kuna mambo mengi ambayo wanajifunza kutoka kwa Bunge la Tanzania chini ya Spika wake Job Ndugai.Pia amesema wataangalia namna ya kuwa na Ofisi Dodoma.Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania amefafanua kikao ambacho kinafanya jijini Dar es Salaam kimewakilishwa na wajumbe mbalimbali na Mwenyekiti wao ni Spika wa Bunge la Kenya.Hivyo kupitia kikao hicho kuna mambo kadhaa watayajadili kwa kina na kwenye suala la bajeti watachambua kwa kina zaidi kwani bajeti hiyo itakuwa ni ya miaka mitatu baada ya kuipitisha.

(Visited 224 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us