ASSAs

ALIYEKUWA MGOMBEA URAIS AWASILISHA MAOMBI KUSAJILI CHAMA KIPYA.

610
0
Share:

bonizacharia.bz@gmail.com

Haikuwa rahisi mtu kuamini kuwa Dkt. Tan Cheng Bock aliyekuwa mgombea wa urais katika mbio hizo za uchaguzi mkuu wa mwaka 2011 kupitia chama tawala cha People’s Action Party (PAP) nchini Singapore angetangaza kurudi tena kwenye siasa ila imekuwa tofauti baada ya yeye kutangaza kuwa ametuma maombi ya kusajili Chama kipya cha Siasa kitakachoitwa Progress Singapore Party.

Taarifa hizo kwa zaidi siku mbili zikiwa zinasambaa, Tan Cheng Bock kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook ameandika kwa urefu ujumbe wa kurudi kurudi upya kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa hivi karibuni huku ikionesha kuongoza kikundi cha watu 12 wa Singapore waliohusika kufungua maombi hayo kwa msajili wakiwemo wakuu wa zamani wa chama tawala cha PAP ambao moja kwa moja hawakutajwa kupitia taarifa hiyo iliyoripotiwa na mtandao wa Channel NewsAsia leo Januari 18, 2019.

“Nimeamua kurudi kwenye Siasa baada ya kutoweka kwa muda mrefu ingawa tunaanzisha Chama kipya, bado tunatarajia kufanya kazi na wengine katika upinzani ambao wanapenda sana kuweka Nchi kwanza kabla ya chama au kujitegemea” Tang aliandika katika chapisho lake kwenye mtandao wa Facebook.

Tang aliendelea kusema kupitia ujumbe huo kuwa “Kwa miaka mingi kikundi chetu kimetembea nchini kukutana na watu wengi wa Singapore kutoka kila aina ya maisha na tulifanya majadiliano nao na kusikiliza wasiwasi wao, hofu zao na kuyasikia pia maumivu yao,

Sisi tulihisi kuwa na hisia zenye wajibu na kujitokeza ili kusaidia shughulikia masuala katika Mazingiara rasmi zaidi kama Bunge, hivyo tuliamua kuunda chama cha siasa ili kuwa sauti ya ziada katika Bunge”.

Dr. Tan Cheng Bock aliongeza kuwa chama chake kinatarajiwa kujenga Singapore ya huruma na ya kidemokrasia ambapo maadili mazuri ya watu wazuri yatahusika na uhuru wa chaguo na uhuru wa kujieleza lazima utalindwa.

Aliendelea kusema kuwa yeye na timu yake wanasubiri kibali kutoka kwa msajili wa vyama na mashirika na baada ya idhini hiyo watafanya mkutano na waandishi wa habari ili kuwaelezea malengo na maono ya chama.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya usajili wa Wizara ya Mambo ya ndani nchini humo wastani wa mchakato wa kusajili Chama katika jamii kikawaida ni karibu miezi miwili.

Inawezekana kuwa ujio wa Progress Singapore Party inaweza kuwa mbadala wa Chama tawala cha People’s Action Party (PAP) kilichoanzishwa tangu mwaka 1954 na kuisaidia Singapore kuwa mojawapo ya Nchi zenye utajiri zaidi ulimwenguni licha ya kuwa mara kadhaa kimekuwa kikilalamikiwa na wapinzani.

Dkt. Tan Cheng Bock mwenye umri wa miaka 78 alikuwa mjumbe wa Bunge la Nchini Singapore kwa miaka takribani 26 toka mwaka 1980 mpaka 2006 na baadae mwaka 2011 alikuwa mgombea aliungwa mkono katika mbio za Urais japo hakushinda ila alishika nafasi ya pili akiwa na kura 738,311 sawa na asilimia 34.85 na aliyeshinda kiti hicho alikuwa ni Tony Tan kwa kura 745,693 sawa na asilimia 35.20.

Source:www.channelNewsAsia.com

(Visited 44 times, 1 visits today)
Share this post