ASSAs

UBALOZI WA UFARANSA WA ZINDUA KITUO CHA ELIMU CHA CAMPUS FRANCE NCHINI TANZANIA

809
0
Share:

Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania wakishirikiana na Serikali ya Tanzania wamezindua kituo cha Campus France kitakacho kuwa  maalum kwa ajili ya kusaidia  Wanafunzi wanaohitaji kupata elimu katika nchi ya Ufaransa, sanjari na utoaji wa mafunzo kabla ya wanafunzi kwenda Masomoni nchini humo.

Kituo hicho kilichozinduliwa na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Nchini Dkt. Keneth Hosea, na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kituo hicho  Dkt. Hosea, amesema anaushukuru ubalozi wa Ufaransa kwa kuanzisha kituo hicho nchini  ambapo amesema  kitarahisisha upatikanaji wa elimu ya lugha ya Kifaransa nchini  pia itasaidia upatikanaji hati ya kusafiria kwa wanafunzi watakao kuwa wanahitaji hati hizo.

“kwa mujibu wa mkuu wa hiki kituo na balozi wa Ufaransa hiki kituo kitatumika kama kiungo kati ya hawa wanafunzi wa kwetu Tanzania wanaotaka kwenda kusoma Ufaransa kitatafsiri taratibu mbalimbali ambazo wanatakiwa wafwate kitatoa Fursa ya kuwaeleza kule Ufaransa kuna nini ili waangalie kilichopo wachague, watapata Fursa ya kufanya udahili na hata taratibu za kusafiri.

Na uzuri ni kwamba mhe. Balozi ametuhakikishia kwamba hata upatikanaji wa Visa itakuwa rahisi kupitia vituo kama hivi tofauti na kuanza kutafuta mwenyewe,” amesema Hosea.

Vilevile Dkt. Hosea ameuomba Ubalozi wa Ufaransa kuongeza idadi ya Watanzania kwenda nchini humo, Pia amemuomba Balozi kuanzisha kozi mbalimbali za muda mfupi kama ufuaji wa umeme wa maji, na uendeshaji wa treni za umeme  zitakazo saidia wanafunzi kunufaika kielimu  na si Lugha ya Kifaransa pekee.

Aidha DK.Hosea amesema kama Kurugenzi ya elimu za juu nchini wameona hii ni fursa iliyo nzuri kama taifa kupata kituo hicho kwani kitasaidia wanafunzi wengi zaidi kufika nchini ufaransa kupata elimu.

 

Msikilize Mkurugenzi wa Elimu ya Juu nchini Dkt. Keneth Hosea akieleza zaidi juu ya uzinduzi wa kituo cha Campus France.

(Visited 149 times, 1 visits today)
Share this post