ASSAs

JUMBA BOVU LA R. KELLY LAMDONDOKEA MAREHEMU MICHAEL JACKSON

1070
0
Share:

Baada ya dunia kusimama baada ya kampuni ya Lifetime kuonesha filamu ya ‘Surviving R. Kelly’ ambayo imegusa ukweli wa vitendo vya unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo, sasa jumba bovu linaenda kumuangukia marehemu Michael Jackson.

Filamu mpya ‘Leaving Neverland’ inatarajiwa kumuacha uchi mfalme huyo wa Pop ikirushwa January 25 mwaka huu. Filamu hiyo imejikita kwenye kuanika vitendo vya ulawiti ambavyo alikuwa akivifanya Michael Jackson kwa wavulana wadogo.

Vijana zaidi ya 30 wametajwa kuzungumza na kuthibitisha kufanyiwa vitendo hivyo, ila ni mmoja ambaye amejitokeza kabla ya kurushwa hewani kwa filamu hiyo: Wade Robson alikuwa mnenguaji wa MJ, amedai kuwa mwimbaji huyo alimlawiti kipindi ana umri wa miaka 7 hadi alipofikisha umri wa miaka 14.

Kijana Wade Robson katikati na Michael Jackson Paris wakati akifanya kazi kwake
Robson aliwahi kufungua shtaka mwaka 2016 na kuishtaki familia ya Michael Jackson lakini mahakama ilitupilia mbali shauri hilo.

(Visited 94 times, 1 visits today)
Share this post