ASSAs

DASICO YAIOMBA SERIKALI KUWATATULIA CHANGAMOTO ZAO

835
0
Share:

Dar es Salaam

Ukosefu wa masoko ya uhakika wa bidhaa zinazozalishwa, gari la kuzolea taka, uchakavu wa majengo pamoja na miundombinu na zana za kufanyia kazi ni miongoni mwa changamoto zinazoukabili ushirika wa viwanda vidogo Dar es Salaam (DASICO LTD)

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa DASICO, Mfaume Yusuf wakati walipotembelewa na Rais wa vyama vya ushirika Duniani akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali lengo likiwa ni kukagua viwanda vya ushirika.

Aidha wameiomba serikali kwa kushirikiana na shirika la ICA kuwatatulia changamoto hizo ili waweze kukuza maendeleo ya kiuchumi pamoja na kujikwamua na umaskini.

Amesema kuwa, lengo la ushirika huo ni kuboresha maisha ya wanachama kiuchumi na kijamii kwa njia mbali mbali ikiwemo uhamasishaji, uwekezaji, uwajibikaji, uwazi pamoja na kusaidia kutoa huduma bora.

Kwa upande wake Rais wa shirikisho la vyama vya Ushirika Duniani (ICA) Dkt,Ariel Guarco amesema kuwa, amefurahi sana kuona kuona viwanda hivyo vikiwa vina endelea na shughuli mbalimbali za udhalishaji.

Aidha amesema, ataendelea kuvisapoti viwanda hivyo, ambapo ameongeza wanachama hao 266 wa ushirika ni sehemu ya watu bill 1 walio katika vyama mbalimbali vya ushirika duniani, ili kuleta maendeleo

Naye Katibu wa chama hicho, Sijaona Mageja amesema kuwa licha ya changamoto zinazowakabilia lakini pia wameweza kufanikiwa kukopeshana mikopo midogo midogo isiyokua na riba pamoja na kuweza kuwalipa mafao wanachama waliostaafu.

Aidha amesema kuwa, ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo kuboresha majengo yaliochakaa panahitajika nguvu ya pesa za kutosha ili kuweza kujenga majengo ya kisasa.

(Visited 47 times, 1 visits today)
Share this post