ASSAs

‘ENDELEENI KUNIOMBEA NISIJE NIKAPATA KIBURI’ RAIS MAGUFURI

827
0
Share:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amefunguka kuwa ataendelea kuwa mtumishi na sio mtawala, kwani anahofu ya Mungu.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Januari 23, Ikulu jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na viongozi wa madhebebu mbalimbali ya dini ili kujadili masuala mbalimbali yanayoendelea nchini, ambapo amewataka viongozi hao waendelee kumuombea katika utekelezaji wa majukumu yake.

Endeleeni kuniombea nisije nikapata kiburi, nitafanya kazi kama Mtumishi na sio Mtawala. Uongozi mara nyingi unawapa watu kiburi wanafikiri wao ndio wao”, amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameongeza kuwa, “Nataka Vyama vyetu viige mfano mzuri wa Viongozi wa dini wanavyoheshimiana na kupendana, kwa sababu jukumu langu mlinipa ni kuilinda amani ya Tanzania, hakuna mtu aliyezuiliwa kufanya mikutano mahali pake”.

(Visited 49 times, 1 visits today)
Share this post