ASSAs

HAMISA MOBETTO ATHIBITISHA MAHUSIANO YAKE MAPYA

2196
0
Share:

Hamisa Mobetto ambaye  ni msanii wa musiki na bongo movies nchini Wiki iliyopita aliingia kwenye headlines Baada ya kudaiwa kuiba bwana wa mrembo aitwaye Tahiya.

Tahiya ambaye ameshawahi kutajwa kuwa kwenye mahusiano na Diamond, alimtuhumu Mobetto kwa kumchukulia bwana ake anayeitwa Alex ambaye anatajwa kuwa mtoto wa Kigogo mmmoja hapa nchini.

kadhaa zilizopita Tahiya  aliposti picha ya Hamisa  Mobeto kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika maneno haya; “Hamisa Mobeto achana na wanaume za watu.”

Baada ya muda mwanadada huyo akaposti tena meseji zao zote alizokuwa wakijibizana na mwanamitindo huyo kwenye mtandao wa WhatsApp ambapo Tahiya alionekana akimsihi Mobeto aachane na mpenzi wake lakini haikusaidia kwani mwisho wa waliishia kujibizana maneno mabaya huku kila mmoja akijiona anaweza zaidi ya mwenzake.

kutokana na skendo hiyo kutawala mitandao ya kijamii Gazeti la Risasi Mchanganyiko lilimsaka Hamisa Mobetto ili kupata Ukweli kwa upande Wake ambapo alifunguka na kusema:

“Mnataka niwaambie nini, mlichokiona ndiyo hichohicho isitoshe mimi siyo mtoto mdogo kwa hiyo naelewa ninachokifanya, sijaiba mwanaume wa mtu ila alikuja mwenyewe na nampenda nifanyeje sasa”.

(Visited 275 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us