ASSAs

WANAFUNZI 57 WAFUTIWA MATOKEO MOROGORO

783
0
Share:

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) leo  wametangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.29 kutoka asilimia 77.09 mwaka 2017 hadi asilimia 78.38.

Wanafunzi 57 wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Tumaini Lutheran Seminari  ya Malinyi mkoani Morogoro wamefutiwa matokeo yao baada ya kubaini shule hiyo kuvujisha mtihani huo.

Mbali na kufuta matokeo hayo, Necta imekifungia kituo hicho cha kufanyia mtihani.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Januari 24, 2019 na Katibu Mkuu mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde wakati akitangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 mkoani Dodoma.

Amesema wameagiza wahusika wote kuchukuliwa hatua wakiwemo polisi waliosimamia.

Dk Msonde ameanza kutangaza matokeo hayo leo saa 5:00 asubuhi.

(Visited 59 times, 1 visits today)
Share this post