ASSAs

WAZIRI UMMY AMWAGA NEEMA SHINYANGA, SERIKALI KUTOA BILIONI 2.5 UJENZI JENGO LA MAMA NA MTOTO

453
0
Share:

Shinyanga

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Amesema kuwa Wizara ya Afya inatarajia kupeleka Shilingi Bilioni 2.5 kwa Ajili ya Ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto Katika Mkoa wa Shinyanga

Kauli hiyo Ameitoa Mapema Leo Alipokua katika Ziara ya Kukagua miradi ya Maendeleo Upande wa Wizara ya Afya Katika Mkoa wa Shinyanga Ambapo Ametembelea Majengo Mbalimbali ya Afya yaliopo ndani ya mkoa huo huku ikiwa Ujenzi unaendelea na unaelekea Kumalizika.

Waziri Ummy Amesema kuwa, lengo la kupeleka pesa hizo ni “Lengo letu ni Kukamilisha Ujenzi wa Majengo ya Awamu ya Kwanza ili tuanze kutoa huduma kwa Wananchi wa Mkoa wa Shinyanga Kabla ya mwisho wa mwaka huu 2019.”

Pia Waziri Ummy Amesema Ujenzi wa Hospitali Mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ambapo Jengo la wagonjwa wa nje (OPD) limekamilika ndani ya wiki 2. Na Kubainisha haya ni Mafanikio Makubwa kwa serikali ya Awamu ya tano Chini ya Rais Magufuli Upande wa Sekta ya Afya Kwani kukamilika kwa Ujenzi wa Jengo hilo unaenda kuwa Msaada Mkubwa Kwa Wananchi wa Mkoa wa Shinyanga

Aidha Ameongeza kuwa, lengo la Ujenzi wa Hospitali hizo ni kuboresha huduma za afya, ambapo Wizara inatarajia kupeleka Fedha kwa Ajili ya Jengo la Huduma za Uchunguzi na Upasuaji katika Wiki Chache Zijazo katika Hospitali ya Shinyanga.

Pamoja na Ziara Hospitali ya Rufaa pia Waziri Ummy Ametembelea Kituo cha Afya Kambarage, kilichopo Manispaa ya Shinyanga ambapo Ujenzi wa Majengo Muhimu kwa Ajili ya Huduma za Uzazi wa Dharura ikiwemo Upasuaji wa Kutoa Mtoto Tumboni (CEMONC) unaendelea Vizuri.

Pia Waziri Ummy Amesema Kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Amemhakikishia Kazi ya Ujenzi itamalizika 15 Feb. 2019, huku Hali ya Utoaji huduma ikiwa Inaridhisha na Dawa muhimu zinapatikana kwa zaidi ya asilimia 90.

“Nimeshuhudia msongamano mkubwa wa wagonjwa, tunaamini tutalimaliza tatizo hili mara tu tukikamilisha ujenzi wa majengo mapya ya (CEMONC) ya kituo hiki na pia tukikamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ambapo tutakabidhi kwa Manispaa ya Shinyanga Majengo ya sasa ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ili kuanzisha Hospitali ya Manispaa”amesema Waziri Ummy.

Hii ni Mwendelezo wa Ziara yake ya Ukaguzi wa Vituo vya Afya na Hospitali ambayo Alianzia Mkoa wa Simiyu, Geita na Sasa Leo Alikuwa Mkoani Shinyanga Katika Kuhakikisha Huduma za Afya nchini zinaboreka, Madawa Yanapatikana na Ujenzi wa Majengo ya Hospitali Yanakamilika kwa Wakati.

(Visited 79 times, 1 visits today)
Share this post