ASSAs

KIONGOZI MASHUHURI WA UPINZANI NCHINI VENEZUELA AJITANGAZA KUWA RAIS

1026
0
Share:

Baada ya maandamano ya kumshinikiza rais Nicolas Maduro kung’atuka madarakani kukumbwa na vurugu, kiongozi mashuhuri wa upinzani Juan Guaido amejitangaza kuwa rais wa mpito.

Bw. Guaido tayari amepata uungwaji mkono kutoka mataifa ya Marekani, Canada, na majirani wa taifa hilo waliyo na ushawishi mkubwa katika kanda ya Amerika kusini kama vile Brazil, Colombia na Argentina.

Muungano wa Ulaya umetoa wito wa kufanywa upya uchaguzi na kuunga mkono bunge la kitaifa litakalo ongozwa na Guaido.

Lakini kuna baadhi ya mataifa yanayomuunga mkono rais Maduro ikiwemo Urusi na China.

Moscow imeonya kuwa hatua ya Guaido, moja kwa moja huenda ikasababisha “uvunjaji wa sheria na umwagikaji mkubwa wa damu”.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ilisema: “Tunaonya kuwa hatua hiyo itakuwa na athari mbaya”

Huku hayo yakijiri msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China, Hua Chunying, amesema kuwa China inapinga ”muingilio” wa nje katika mzozo wa Venezuela.

“China inaunga mkono mikakati ya kulinda uhuru wa Venezuela wa kujitawala” alisema.

“China itaendelea kushikilia msimamo wake wa kutoingilia masuala ya ndani ya matifa mengine’.”

Uturuki, Iran, Mexico, Cuba na mataifa mengine pia yana muunga mkono Maduro.

Kwa mujibu wa msemaji wa mamlaka ya urais wa Uturuki Ibrahim Kalin, Rais Recep Tayyip Erdogan amempigia mwenzake Nicolas Maduro na kumhakikishia kuwa Uturuki itasimama nae: ”Ndugu Maduro, Simama imara, tuko nawe kwa hilo.”

Msemaji huyo alitumia hashtag #WeAreMADURO.

Lakini hali ya taharuki inayoshuhudiwa katika ulingo wa siasa za kimataifa huenda isibadilike huku maafisa wa Marekani na Venezuela wakitupiana cheche za maneno.

Muda mfupi baada ya Rais Donald Trump kumtambua Guaido kama kiongozi wa muda wa Venezuela, Maduro alisema kuwa amekomesha mara moja uhusiano wa kidiplomasia na wa kisiasa na Marekani.

Alisema “Wafanyikazi wote wakidiplomasia na ubalozi wa Marekani nchini Venezuela” wana saa 72 hours kuondoka nchini humo.

Akijibu tamko hilo waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo, amesema kuwa Marekani haitafanya mashauriano ya uhusiano kidiplomasia kupitia serikali ya Maduro isipokua Guaido.

(Visited 67 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us