ASSAs

TUHUMA ZA ZITTO KUTAKA KUJITEKA NI NZITO, AELEZE UMMA KWA NINI?

919
0
Share:

 

Taasisi ya Kizazi Cha Kuhoji Afrika (KICHAKUA) chenye makazi yake jiji Dar es Salaam kimetoa walaka mzito wa kuhoji tuhuma inayomuandama mwenyekiti wa chama cha ACT wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, huku walaka huo ukimsisitiza Zitto kujitokeza na kujibu tuhuma hizo.

Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia Chama cha upinzani Chadema na washirika wake wakitumia mbinu ya ama watu kupotea au kuuawa katika jinai za kawaida ambazo zimekuwepo tangu zama lakini wao wakianza kuzitumia kama mbinu ya kisiasa bila kuzingatia misingi ya uchunguzi.

Wakati hata zamani watu walikuwa wakipotea kwa sababu mbalimbali au kuuawa kwa sababu mbalimbali, inaonekana mbinu ya kutishiwa kuuawa, au watu kutoweka kwa sababu zao sasa imekuwa kiki ya kisiasa si tu Chadema bali hata ACT; tunasikitishwa suala hili sasa linavyogeuka kuwa mtaji wa wanasiasa na kutaka kuichafua Serikali bila sababu

Tunayo masikitiko makubwa kuona wanasiasa kama Zitto Kabwe nao wanaingia katika mkumbo huu baada ya kila hoja anayoishika kuonekana haina nashiko.

Taarifa zilizoenea ni kuwa sasa mwanasiasa huyo anataka kujitengenezea au kuna namna atatengenezewa na watu wake au wakubwa zake walioanza kumchoka ili litokee tukio la kujeruhiwa au kutishiwa maisha ili ajijengee mtaji wa kisiasa.

Taarifa na tuhuma hizi ni nzito na mbaya kwa Taifa hivyo sisi vijana wa Kizazi cha Kuhoji Afrika tunamtaka Mhe. Zitto Kabwe kujitokeza na kutoa ufafanuzi wa tuhuma hizi mbaya zinazoweza kuichafua nchi.

 

Tuhuma hizi hazipaswi kupita bila kukemewa hasa ikizingatiwa kuwa hii inaanzakuwa fasheni kwa wanasiasa wa upinzani.

Mbunge Tundu Lissu hata akiwa hajahojiwa na wachunguzi amekuwa akilaumu Serikali hadi aliposhindwa rasmi kuthibitisha madai yake mbele ya Mtangazaji wa BBC.

Lakini ikumbukwe, na cha ajabu, wanasiasa kama Zitto, hii ya kujitungia uongo kuwa watauawa au wanatishiwa ni staili yao tangu zamani.Wamesahau tu.

Wakati Lissu akiwa mwanaharakati wa madini alipata kutishiwa na mabeberu wa madini hadi akaenda kusoma nje, Zitto naye akiwa Chadema alipata mara kadhaa kusema anategeshewa kuuawa.

Lakini leo Lissu kasahau maadui wa wakati huo waliokuwa na usongo naye na Zitto ametoka Chadema lakini sasa amewakumbatia wale wale aliowatuhumu kuwa wanataka kumuua kwa kuungana na Chadema.

Sasa Zitto kaibua madai kuwa Tiss au watu asiowataja wanataka kumuua.

Kama aliwatuhumu Chadema na leo ndio marafiki zake ni aidha Zitto ni mkweli kwa hiyo anapaswa kutoa vielelezo kuanzia matishio aliyokuwa nayo Chadema ili hata sasa akidhurika watu watrace maadui zake au ni muongo wa kutupwa anayetumia staili hii ya kudai kuuawa kama kiki ya kisiasa.

Ndio maana, kwa utata huo, tumeshawishika kujitokeza kumtaka Ndugu Kabwe atoke hadharani kuueleza umma kipi ni kipi?Lissu tutamsubiri apone aje aeleze anadhani wale waliomkimbiza mwanzo hadi akaenda kusoma nje na akarudi akaanza kuwazodoa tena katika mabeberu wa madini anadhani alimalizana nao?

Je, ni kweli Zitto naye anatishiwa? Kama ni kweli ni kina nani walimtisha akiwa Chadema?waligombana naye nini?Walichogombana kimekwisha? Kama ndio kimekwisha vipi?

Je, kama ni kweli anadhani maadui zake ni nani hasa?Alishamalizana na maadui zake waliotaka kumuua akiwa Chadema?Kwenye madini ambako amekuwa akitumika hana maadui?Kwa nchi anakopita na kutuma taarifa nyingine zikigeuka za uongo na kuwaudhi waliomtuma licha ya kumlipa hela nako anadhani hana maadui?Anatengeneza hitimisho gani hata pale ambapo jambo halijatokea anaanza kuilaumu Serikali?Je, anashiriki hicho anachokiita mipango mibaya dhidi yake? na labda la mwisho; anajua maumivu aliyowasababishia makumi ya mabinti aliowatelekeza?Hadhani kwamba hawa nao ni maadui?Kwa nn shida zake kama zipo zote anakimbilia kulaumu na kutaka kuchafua nchi?

(Visited 92 times, 1 visits today)
Share this post