ASSAs

WAZIRI UMMY AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UN WOMEN KANDA YA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA

346
0
Share:

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amekutana na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Dkt. Izeduwa Derex-Briggs kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake(UN Women)  kwa lengo la kumpa taarifa ya Mkutano wa 63 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake duniani utakaofanyika Mjini New York Mwezi  Machi Mwaka huu.

Aidha Waziri Afya pamoja na Kiongozi huyo walifanya mazungumzo na kubadilishana mawazo kuhusu maeneo ambayo shirika la UN Women linayafanyia kazi kwa kushirikiana na serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Katika kikao cha muda mfupi ofisni kwa Waziri Ummy kiongozi huyo pia alimwalika Waziri Ummy kushiriki katika Mkutano wa Afrika wa  kujenga msimamo wa pamoja ambao ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano  Mkutano wa 63 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake duniani utakaofanyika Jijini Cairo  mwezi Februari mwaka huu.

Bi. Derex-Briggs pia ameitaka Tanzania kuhakikisha inaingiza masuala ya Jinsia katika taarifa yake itakayotoa katika Mkutano wa kimataifa wa Jukwaa la Juu la Kisiasa (High Level Political Forum) utakaofanyika  Mwezi  Julai ,9-18  Jijini New York Marekani mwaka huu.

Wakati huohuo Waziri Ummy Mwalimu amemwambia Mkurugenzi huyo kuwa Wizara yake imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Shirika la UN Women na kusema vipaumbele vyake kama Waziri mwenye dhamana imekuwa ni kuhakikisha wanawake wote wanapata huduma ya kujifungua salama katika vituo vya Afya.

Aidha Waziri Mwalimu amesema maeneo mengine ya kipaumbele kwasasa ni uwezeshaji wanawake kiuchumi, juhudi za kuhakikisha kunakuwepo uwakilishi wanawake katika maamuzi ya kisiasa unaendelea kufikia 50/50 lakini pia kupunguza mimba na ndoa za utotoni ambazo ni kikwazo kwa wasichana wengi kufikia ndoto zao.

Kuhusu suala la uwezeshaji wa wanawake kiuchumi Waziri Ummy amesema kuna asilimia 4 ya fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri zimekuwa zikitolewa kwa ajili kuwazesha wanawake kiuchumi lakini kuna idadi dogo ya wanawake wanaojitokeza kuomba mikopo hiyo.

Katika sula la uwezeshaji wa wanawake kisiasa Waziri Ummy bado kuna changamoto ambazo zinahitaji kufanyia kazi ili wanawake waweze kujitokeza kwa wingi kushiriki katika masuala ya kisiasa kwani uwakilishi wanaume bungeni bado ni mkubwa ukilinganisha na wanawake.

Naye mwakilishi wa shirika la UN Women Nchini Tanzania Bi. Hodan Addou amemwahakikishia Waziri Umy kuwa Shirika lake litaendelea kuchangia katika Maendeleo ya Wanawake Nchini kwani mpaka sasa limechangia katika Maeneo yote ya vipaumbelea kwa kushirikiana na Wizara.

Aidha Bi. Derex-Briggs anaitembelea Tanzania kwa ziara ya kikazi tayari ametembelea Ofisi ya Taifa ya Takwimu na amekuwa Jijini Dodoma kutembelea Bunge la Tanzania ambapo amepata fursa ya kuongea na baadhi ya wabunge wanawake na kubadilishana nao mawazo  kuhusiana na mstakabali wa masuala ya wanawake.

(Visited 20 times, 1 visits today)
Share this post