ASSAs

DC MJEMA AAGIZA KUSAKWA WANAFUNZI 6000 AMBAO HAWAJARIPOTI SHULE

701
0
Share:

Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ametoa agizo la mwezi mmoja kwa Ofisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ilala kuwasaka wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wamefaulu hawajaripoti Shule.

Mjema ametoa agizo hilo Dar es Salam leo wakati wa ziara yake ya Elimu Sekondari kukagua ukarabati wa majengo ya sekondari na ujenzi wa majengo mapya Manispaa ya Ilala.

“Nakuagiza Kaimu Ofisa Elimu Sekondari Steven Petro ukakae na Ofisa Elimu wako mufanye oparesheni ya kuwasaka wanafunzi 6,2,74 ambao mpaka sasa bado wajaripoti shule tujue sababu zake muende kwa wazazi wao na kama wameolewa wazazi wachukuliwe hatua “amesema DC Mjema.

Mjema aliwataka walimu wa Sekondari wafuatilie kwa wazazi wao Serikali iweze kujua kwanini wanafunzi mpaka leo hawajaripoti kusoma, mpaka kufikia mwezi machi mwaka huu anataka apewe taarifa za kujitosheleza kwa wanafunzi wote ili Serikali iweze kuchukua hatua.

Akielezea ufaulu wa darasa la saba mwaka 2018 wanafunzi ambao wamekwenda Sekondari 21,400 na wote wamechaguliwa kwenda kidato cha kwanza mwaka 2019 kati ya wnafunzi hao wavulana 10171 na wasichana 11229.

Ameongeza kuwa, idadi hiyo ni kubwa ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2017 walikuwa 19,236 lakini ameshangazwa na mapokezi ya wanafunzi January 7 hadi leo January 28 wanafunzi ambao wameripoti Shule 15,126 kati yake wavulana ni 7,222 na wasichana 7,904 sawa na asilimia 70 bado wanafunzi 6,274 kuripoti Shule hadi leo.

Wakati huo huo, DC Mjema ameagiza kukamatwa kwa kiongozi wa wafanyabiashara wamachinga wa Kata ya Gongolamboto Kristopher Kidiga kwa kulalamikiwa kutoza 10,000 fomu za vitambulisho vya Rais Magufuli kinyume cha uratatibu wa maagizo ya Serikali.

Aidha, amesema Rais John Magufuli alitoa agizo wafanyabiashara wote wamachinga wapewe vitambulisho hivyo kwa gharama ya shilingi 20,000 si vinginevyo, hivyo amelitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi kuanzia leo kuwakamata watu wanaohamasisha wafanyabiashara wa Kariakoo wasinunue vitambulisho vya Rais akidai vinatolewa bure.

Kwa upande wake, Ofisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ilala Stephen Petro amesema maagizo yaliotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema watayafanyia kazi na kuleta taarifa ofisi ya idara elimu sekondari ina taarifa ya wanafunzi 123 wa kidato cha kwanza wamefaulu Wapo shule binafsi.

Petro amesema, Halmashauri hiyo ina jumla ya kata 36 kati ya kata hizo 13 hazina Shule za Sekondari za kata hivyo kusababisha msongamano katika shule za kata zilizopo Manispaa hiyo, ambapo jumla ya Shule za Sekondari 100 zilizopo kati ya hizo 52 za Serikali moja haijasajiliwa na 48 za binafsi.

Amesema kuwa, kutokana na changamoto ya miundombinu iliyopo katika Manispaa hiyo wamelazimika kuazima madarasa katika shule za msingi Zavala, uamuzi, na Kinyamwezi ambazo hazijasajiliwa ni mpya .

(Visited 49 times, 1 visits today)
Share this post