ASSAs

JB AMKINGIA KIFUA HAJI MANARA

340
0
Share:

Sakata la mashabiki wa Simba kumshambulia Afisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara kutokana na matokeo mabovu limeendelea kuchukua sura tofauti baada ya muigizaji wa Bongo Movies nchini, JB kulizungumzia Afisa Habari huyo.

JB amesema kuwa Manara anasaidia kuitangaza ligi na klabu ya Simba kwahiyo ni jambo la kupongezwa kwakuwa hapa nchini ni ngumu watu kushawishika kujaza uwanja kwa mechi za kawaida.

Sisi ligi yetu haifanyiwi ‘promotion yoyote’ anachofanya Haji ni kitu kikubwa sana kwa mpira wa Tanzania, kwa kupiga tuu kelele zake inasaidia uwanja kujaa mara nyingi sana. Kwahiyo wangepatikana watu wa hivi wanne au watano ambao kila saa wanaongea mpira inasaidi watu kujaa uwanjani“, amesema Manara.

Kungelikuwa na wasemaji wengine wa upande wa pili kama Azam, Yanga au Mbao FC ambao wangeongea kwa namna nyingine yeyote ingesaidia. Mimi namsifia Haji na nasema ukweli, sijawahi kuona msemaji ambaye anaongea vizuri kama Haji, mtu anayemsema vibaya haelewi kitu anachokifanya“, ameongeza.

Haji manara ameelezea masikitiko yake makubwa kwa namna ambavyo mashabiki wa Simba walivyomshambulia kutokana na matokeo mabaya ya timu hiyo katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na mashindano ya SportPesa yaliyomalizika hivi karibuni.

Manara alisema, “kazi yangu mimi kubwa ni kuisemea Simba popote pale, nimekuwa nahakikisha Simba inajaza uwanja na jukumu la kufanya vizuri uwanjani ama la ni la timu. Nimesema Simba itamfunga Barcelona ni kwaajili ya kuhakikisha mashabiki wanajaa uwanjani, kwani mimi sijui kuwa Messi ni zaidi ya mchezaji wa Dunia?, lakini nilikuwa nafanya kwa ajili ya kuhakikisha mashabiki wanakuja uwanjani“.

Mimi sitokaa milele kama msemaji wa Simba, ila nitabaki milele kama shabiki wa Simba, haimaanishi kuwa Simba ikifungwa ndiyo nishindwe hata kufanya mambo yangu mengine“, aliongeza Manara akiwajibu mashabiki ambao walikuwa wakimkosoa alipokuwa akifanya maandalizi ya hafla yake.

(Visited 22 times, 1 visits today)
Share this post