ASSAs

JAJI MKUU ABAINISHA KUKATALIWA OMBI NA RAIS MAGUFULI

411
0
Share:

Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Profesa Ibrahim Juma amebainisha kupeleka maombi ya kupatiwa idadi ya Majaji wapya 30, ambao wangewezesha kupunguza mzigo wa kesi za mahakamani ambapo kwa sasa uwiano wa kila Jaji mmoja ni kusimamia kesi 562.

Akizungumza kwenye hafla ya kuwaapisha majaji 15 Ikulu Jijini Dar es salaam Profesas Juma amesema bado Mhimili huo wa mahakama unakabiliwa na changamoto ya Majaji ambao wa sasa wamekuwa wakipewa mzigo mzito wa kuhukumu kesi.

Jaji Mkuu amesaema, “kuna siku moja ulinipigia simu ukaniuliza hivi unahitaji majaji wangapi ili kupunguza mrundikano wa mashauri mahakamani nikakujibu kuna majina zaidi 65 nikakuomba walau 30 ukacheka sana“.

Ujio wa majaji 15 utashusha mzigo wa kwenye kesi, asubuhi ya leo kila Jaji angebeba mashauri 568 kwa mahesabu hadi Disemba 2018 lakini baada ya kuwapata hawa mzigo utakuwa 462 ila ni mzigo bado ni mzito” ameongeza Profesa Juma

Aidha amesema lengo la mahakama hiyo ni kuwa na zaidi ya Majaji 150 huku akiwataka kuwa watiifu wa sheria bila ili kuwa mfano bora.

(Visited 20 times, 1 visits today)
Share this post