ASSAs

WAVUVI WAMLILIA RAIS MAGUFULI, WAOMBA KUONANA NAYE WAMWELEZE MATESO WANAYOKUMBANA NAYO

597
0
Share:

Makamu Mwenyekiti wa umoja wa Wavuvi Wadogo nchini Salehe Msiani amemuomba Rais Magufuli kuiangalia Sekta ya Uvuvi, huku akidai kuwa sekta hiyo haipewi kipaombele katika serikali.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na Lemutuz Blog bw.Msiani amesema kuwa zipo changamoto nyingi wanazokumbana nazo ambapo amesema suala la utatuzi wa changamoto hizo umekuwa ni tatizo, pia amemuomba Rais kuwapatia nafasi ya kukutana naye ili waweze kumueleza zile changamoto wanazozipitia.

“Kwakweli Sekta ya Uvuvi inadharauliwa sana na inachangamoto kubwa sana kwetu sisi, mvuvi anabeba watu wengi sana lakini leo hapa ukiangalia wamama wamekaa hapo chini wamekaa hapo hakuna samaki, muuza mfuko leo hauzi mama lishe hauzi watu wenye daladala wamepaki magari yao kwamaana wachuuzi hakuna, Sekta ya uvuvi inabeba sekta nyingi sana katika nchi hii.

Sisi tunamuomba Rais anakuja hapa anazungumza na wavuvi sawa lakini viongozi sisi changamoto zetu zinaishia katika maandishi na hazishughulikiwi ipasavyo lakini kama atazijua kero basi atatuokoa kwamaana tunajua yeye ni Rais mpenda haki na Rais wa wanyonge atusikilize atuite atusikilize kero zetu” amesema Bw. Msiani.

Januari 28,2019  Fungamano la Vyama vya Sekta ya Uvuvi wa Ukanda wa Pwani Tanzania lilitangaza mgomo wa wavuvi lengo likiwa ni kuishinikiza Serikali ya Tanzania kukomesha mauaji ya Wavuvi baharini.

Tamko hilo lililosomwa na Mwenyekiti wa Fungamano hilo Mohammed Saidi, ambapo alisema licha na kuuawa Wavuvi bali kumekuwa na mateso mengi yanayowakumba wavuvi ikiwemo Vipigo pamopja na kuzuia kutumia nyavu za matundu.

 

(Visited 34 times, 1 visits today)
Share this post