ASSAs

RAY AMVAA HAJI MANARA

723
0
Share:

Muigizaji nguli wa Bongo Movies, Vicent Kigosi ‘Ray’ amemtaka Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara kuwaambia ukweli mashabiki wa timu hiyo badala ya kuwaaminisha kuwa watashinda kila mechi na hatma yake inadhalilishwa kwa vipigo vya aibu.

Ray amesema kuwa Manara anatakiwa kuacha kuwajaza upepo mashabiki wake na mwisho timu inafungwa kwani iko siku  wanatamchoka na watamvaa.

Mimi nawaambia, mpira una matokeo matatu, wape watu 50/50. Manara usiwajaze upepo mashabiki wako halafu timu inakuja kufungwa, siku moja watakuchoka watakuja kukuvamia, usiwaaminishe watu asilimia 100 kuwa mnashinda kama Chelsea na Everton, wewe uwezo huo huna“, amesema Ray.

Pia Ray amesema kuwa klabu ya Simba bado ni ‘underdog’ na ushindi walioupata dhidi ya JS Saoura katika Uwanja wa Taifa klabu hiyo ilibahatisha huku akiwataka kujiandaa na kichapo kingine kikubwa kutoka kwa Al Ahly.

Simba ni ‘underdog’ na yule mwarabu walimbahatisha tuu hapa na wajiandae na kichapo kingine huko Misri, tano zilezile tena ‘Khamsa’, nawaambia hivyo Simba“, ameongeza.

Kwa siku za karibuni, morali ya mashabiki wa Simba imeendelea kuporomoka kufuatia matokeo yasiyoridhisha ya klabu hiyo. Baadhi ya mashabiki wameendelea kurusha lawama zao kwa wachezaji, wakiamini kuwa uwezo wao wa kupambana uwanjani umeshuka licha ya kuwa wanaishi maisha mazuri.

Mashabiki wengine wanatupa lawama zao kwa uongozi, akiwemo Haji Manara kutokana na maneno yake ya kupitiliza kuwa yanasababisha wachezaji kujiamini kupita kiasi hadi kupelekea kudharau baadhi ya mechi. Lakini mwenyewe Haji Manara amejitetea kuwa kazi yake ni kuhamasisha mashabiki kuisapoti timu yao na si vinginevyo.

 

CREDIT: EATV

(Visited 52 times, 1 visits today)
Share this post