ASSAs

SIKU ZA MIFUKO YA PLASTIKI ZAHESABIKA NCHINI

777
0
Share:

Serikali imedhibitisha kuwa katika hatua za mwisho za mazungumzo ili kuhakikisha wanamaliza matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam Mhandisi Viwanda Ofisi ya Makamu wa Rais Dodoma Julius Enock, katika mjadala juu ya athari za uchafuzi wa taka za plastiki ulioandaliwa na Ubalozi wa Ufaransa nchini, amesema bado ipo changamoto kubwa katika matumizi ya plastiki ambapo amesema endapo nchi itaacha mifuko kuendelea kutumia baada ya miaka mitano nchi itakuwa katika adhari kubwa zaidi.

Enock amesema mpaka sasa plastiki zinazotengenezwa ndani ya nchi ni 30% ambazo hizi zinatengenezwa na viwanda vya ndani na 70% zinatengenezwa katika viwanja vya nje, ambapo amebainisha plastiki nyingi zinazoingia nchini ni zile zinazoingia kwa njia zisizo salama.

“kikubwa tulikuwa tunazungumzia suala la changamoto za plastiki nchini na ni kitu ambacho tukikiacha ifikapo 2020-2025 adhari zitakuwa mbaya zaidi, kama serikali tupo katika hatua za mwisho kabisa kufanya maamuzi ya kuzuia matumizi ya plastiki nchi za majirani zetu wamefanikiwa ila Tanzania ndio imekuwa kama jalala, kitu ambacho sio kizuri tuna andaa program ambayo tutatengeneza kanuni ambayo itaweka sheria ya kudhibiti uingizwaji wa plastiki nchini,” amesema Enock.

Aidha Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili Hussein Mohamed amesema yapo madhara mengi yatokanayo na matumizi ya plastiki ambapo alisema mpaka sasa utafiti uliofanyika japo haujadhibitishwa unaonyesha matumizi ya plastiki ndio chanzo cha magonjwa kama ya Kansa, maini, matatizo ya mfumo wa uzazi.

Mohamed ameiomba serikali itafute mbadala madhubuti wa plastiki ili kuweza kudhibiti mfumuko wa magonjwa nchini.

“plastiki ina madhara mengi sana sema tatizo linachelewa kuonekana, yapo matatizo makubwa ambayo watafiti tumeona ni kama kansa, matatizo ya mfumo wa uzazi japo kuwa tunashindwa kusema moja kwa moja, kikubwa tunaiomba serikali iliangalie hili kwa kutafuta mbadala wa plastiki” amesema Mohamed.

Naye Mkurugenzi wa taasisi ya Nipe Fagio Ana Rocha amesema anaamini kutokomeza plastiki na takataka nchini kutafanikishwa na wananchi kwa kuwa ndio wenye uwezo mkubwa wa kukataa kutumia plastiki kwa kuipigia kelele serikali na ikaelewa tatizo.

“sisi tunauwezo mkubwa sana kama wananchi tunaweza kusimamisha matumizi ya plastiki, na plastiki kubwa ambayo sisi tunaitumia ni mifuko kwa hivyo tukiamua kuacha hata uzalishaji wa mifuko hiyo utapungua na mwisho wa siku utaisha kabisaa,” amesema Rocha.

Katika mjadala huo uliohusisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali, ikiwemo DUCE,UDSM  pamoja na chuo cha MUHAS, pia ilihusisha wakufunzi kutoka katika vyuo mbalimbali nchini, mabalozi pamoja na wageni wengine walipata fursa ya kuangalia video iliyo onyesha adhari za matumizi ya plastiki ndani ya bahari pamoja na kutoa fursa kwa wageni kuuliza maswali kwa wageni lengo likiwa ni kupata uelewa wa kutosha juu ya madhara ya plastiki kwa jamii.

(Visited 64 times, 1 visits today)
Share this post