ASSAs

HATIMAE MO J ATANGAZA NDOA NA GIGY MONEY

1566
0
Share:

LICHA ya penzi lao kuwa na migogoro kila wakati, mtangazaji wa Choice FM, Mourad Alpha ‘Mo J’ ameibuka na kutangaza kumuoa mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye ni mzazi mwenzake, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ili kutimiza ahadi waliyowekeana.

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Mo J alisema mpango wa kumuoa Gigy Money alikuwa nao kwa muda mrefu kwa sababu kwanza ni mwanamke aliyethubutu kubeba mimba yake kwa kipindi chote cha miezi tisa hivyo kumpa heshima ya kuitwa baba.

“Gigy ndiyo sababu ya mimi leo kuitwa baba, nampenda sana hayo mambo mengine ya migogoro huwa yanatokea tu kwa bahati mbaya, namshukuru Mungu Gigy ni muelewa hivyo huwa tunaongea na kumaliza tofauti zetu wenyewe, kwa hiyo Mungu akipenda kabla huu mwaka haujaisha nitafu nga naye ndoa,” alisema Mo J.

(Visited 125 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us