ASSAs

HIVI NDIVYO SIMBA WANAVYOJIVUNIA

1449
0
Share:

Klabu ya soka ya Simba kupitia kwa kiungo wake Haruna Niyonzima amesema mpaka jana Februari 1 walipomaliza maozezi ya mwisho wachezaji wote walikuwa salama na tayari kwa mchezo huo wa leo.

Niyonzima amesema wanajivunia hilo kwasababu inampa uwanja mpana mwalimu Patrick Aussems, kuchagua wachezaji wa kuwatumia na hatimaye timu yake kupata matokeo mazuri tofauti na wengine wangekuwa majeruhi.

Niyonzima pia amesema wachezaji wanajivunia uongozi wao kwa kuwapeleka mapema nchini Misri jambo ambalo limewasaidia kuzoea hali ya hewa ambayo kwasasa ni ya baridi kali.

”Naweza kusema kuwahi kuja hapa kumetusaidia sana maana baridi ni kali mwanzo lilitusumbua sana lakini sasa kwa siku tatu tulizokuwa hapa tumezoea”, amesema Niyonzima.

Simba inacheza na Al Ahly leo kwenye mchezo wa kundi D, ambao utapigwa saa 4:00 usiku kwenye uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria ambao unaingiza takribani watazamaji 86,000.

(Visited 146 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us