ASSAs

KOCHA WA YANGA AFUNGUKA KUHUSU MSAMBULIAJI WAKE KUPOTEZA KIWANGO CHAKE

1258
0
Share:

LICHA ya kufunga bao la kusawazisha, lakini Kocha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera amesema kuwa mshambuliaji wake, Heritier Makambo kwa sasa amepoteza kiwango chake ambacho alikuwa nacho awali.

Kauli hiyo, aliitoa dakika chache baada ya mchezo wa Kombe la FA kumalizika kwa Yanga kuwafunga Biashara kwa penalti 5-4 baada ya timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Katika mchezo huo, mabao ya Yanga yalifungwa na Mrundi, Amissi Tambwe na Makambo, kabla ya kwenda kwenye penalti na kufanikiwa kufuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo. Akizungumza na Championi Jumamosi, Zahera alisema kuwa tangu Makambo arejee kutoka DR Congo, kiwango chake kimeshuka ghafla katika michezo
miwili aliyoicheza ukiwemo wa SportPesa waliocheza na Kariobangi Sharks na ule wa juzi.

“Yule Makambo ninayemfahamu siyo huyu wa hivi sasa, amepunguza umakini katika ufungaji wa mabao ikiwemo katika mchezo huo na Biashara ambao ninaamini kama angekuwa makini, basi mchezo huo tusingefikia hatua ya penalti. “Ninaamini atabadilika baada ya kukaa na kuzungumza naye lakini kila mtu ameona kiwango cha Makambo katika mchezo huu wa Kombe la FA, amecheza katika kiwango cha chini tofauti na michezo yote aliyoicheza,” alisema Zahera.

(Visited 108 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us