ASSAs

MBOWE APEWA MASHARTI NA MKUU WA WILAYA

807
0
Share:

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, amempa ruhusa ya kufanya mikutano ya hadhara Mbunge wa Jimbo la Hai ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na kumtaka Mbunge huyo kuzungumzia ajenda ya maendeleo.

Lengai Ole Sabaya ametoa kauli hiyo akiwa Mkoani Kilimanjaro wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Hai katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais John Magufuli.

Akizungumza na baadhi ya wanachama wa CCM Wilayani Hai Mbele ya Mwenyekiti wa UVCCM, Kheri James, Ole Sabaya amesema Mbunge anaruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara jimboni kwake ila aombe kibali kutoka kwa Jeshi la Polisi.

Kama Mbunge anataka kufanya siasa aje kufanya siasa hapa awataarifu polisi aje kufanya mkutano wa hadhara na mkutano usiwe unazungumzia mambo mengine zaidi ya maendeleo aliyowaahidi watanzania.” amesema Sabaya.

Niseme hakutakuwa na Mbunge mwingine wa maeneo mengine atakayekuja kufanya mkutano ndani ya Wilaya ya Hai wananchi wenyewe ndio wanaojua matatizo ya watu wa Hai” ameongeza Sabaya.

(Visited 55 times, 1 visits today)
Share this post