ASSAs

PAUL MAKONDA AWAJIA JUU WASANII WANAOMTUMIA STEVE NYERERE KAMA DARAJA WANAPOKUWA NA SHIDA

1114
0
Share:

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda amewatolea povu wasanii wote ambao wamekuwa na tabia ya  kumsema vibaya Steve Nyerere na hata kumuita bwana mipango   na kwamba ni tapeli na kusahau kuwa wao ndio wamekuwa wakimtumia huyo huyo kuomba misaada kwake.

Paul Makonda anasema kuwa amekuwa akichukizwa sana na tabia ya baadhi ya wasannii kufanya na kuongea kashaf kwa steve nyerere wakati wasanii wengi sana wanapokuwa na shida wamekuwa wakimtumia msanii huyo ama daraja ya kutaka kufanikisha matatizo yao.

Akitolea mfano, mkuu wa mkoa anasema kuwa wapo waliowahi kukamatwa na wamekuwa na tabia ya kumuomba steve kuongea na mkuu wa mkoa ili wapate wepesi wa makosa yao.

Ikumbukwe kuwa steve nyerere amekuwa akiandamwa mara nyingi hasa kutokana na kujitoa kwake huku wengi wakisema amekuwa akifanya hivyo kwa ajili ya maslahi yake.

(Visited 83 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us